WANAMUZIKI Diamond na Yamoto Band wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Siku ya Msanii litakalofanyika Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo katika ukumbi wa Maelezo , Ofisa Uhusiano wa Siku ya Msanii (SYM) , Peter Mwendapole, amewataja wasanii wengine watakaokuwapo ni pamoja na mwanamitindo Asia Idarous, Miss Tanzania, Miss Universe na wasanii toka Kenya, Erick na Fred Omondi huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Gharib Bilal.
Post a Comment