Tukio
la ajabu na la kushangaza limetokea huko nchini Nigeria baada ya
kijana mmoja kukutwa akiwa amekufa kaburini,kijana huyo alikumbwa na
umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la
marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Saturday Tribune wa Nigeria, tukio hilo limetokea
katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa
amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.
Mmoja
wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na marafiki
zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo lakini baada ya kuona
mwenzao amenaswa ndani ya kaburi walikimbia na kumuacha akihangaika
kujinasua,lakini jitihada zake ziligonga mwamba mpaka pale umautiulipo
mkuta.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi huku kichwa chake kikiwa kimefunikwa na tope.
Mtandao
wa Saturday Tribune ulibahatika kuongea na kamishina wa Jeshi la
Polisi wa eneo la Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi
watafanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa
kilipelekea kijana huyo kupoteza maisha.
Msemaji
wa jeshi hilo aliongeza kuwa mpaka sasa jeshi lake bado halijathibisha
kwamba tukio hilo limetokana na masuala ya kishirikina.
Post a Comment