Halmashauri ya manispaa ya Ilala imesema kuwa majani ya mapapai si tiba ya ugonjwa wa dengue hivyo ni vyema wananchi wakafika hospitalini kupatiwa dawa kuliko kudanganywa na waganga wa jadi....
Kauli
hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na kaimu mganga mkuu wa
manispaa ya Ilala, Dr Willy Sango, wakati wakitoa mafunzo kwa
wenyeviti wa serikali za mitaa jinsi ya kuelimisha wananchi
jinsi ya kujikinga na homa ya dengue...
Dr
Sango alisema ugonjwa wa dengue hauna tiba wala chanjo bali
wanatibu dalili za ugonjwa huo tu, hivyo ni vyema wananchi
wakachukua tahadhari ya kujikinga nao....
Pia
aliwataka waganga wa jadi kuacha kuwadanganya wananchi kwa
kusema kuwa majani ya papai yanatibu kwani hiyo si kweli na
hayajathibitishwa na wataalam wa afya...
Alisema
kuwa mtu akiugua anatakiwa aende hospitali kwanza, asiende
kutumia dawa bila kupima kwani hiyo ni hatari, hivyo wananchi
wanatakiwa kufika hospitalini kupima ndipo waanze kutumia
dawa....
Hata
hivyo alisema, wenyeviti wa serikali za mitaa wanatakiwa
kuhakikisha wanasimamia vizuri maeneo yao pamoja na kushauri
wananchi kwenda hospitali na kuacha kudanganywa na majani ya
mapapai....
"Majani
ya papai si dawa ya dengue wala hayajathibitishwa na mpaka
sasa hakuna dawa ya ugonjwa huo. Tunacho tibu ni dalili zake
tu, hivyo wananchi msidanganyike na waganga wachache wanaotaka
pesa," alisema Dr Sango
Pia
alisema kuanzia kesho, dawa zitaanza kupuliziwa mtaa mmoja
baada ya mwingine ili kuua mazalia ya mbu hao wanaoeneza
ugonjwa huo....
Hata
hivyo alisema kuwa watu wanaopulizia dawa hizo wanatakiwa
kufika katika ofisi za serikali za mitaa ili watambuliwe
kwanza ndipo waendelee na zoezi hilo.
Post a Comment