Abdallah Mrisho akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu tukio hilo.Wanahabari wakiwa kazini.
KAMPUNI ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa shindano la
kumtafuta mwanamke bora wa mwaka ambaye mchango wake wa maendeleo kwa
jamii umewazidi wenzake, imethibitisha fainali hizo kufanyika keshokutwa
Jumamosi.Akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Atriums, Jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Abdallah Mrisho, amesema fainali hiyo itafanyika mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye atawakabidhi tuzo washiriki wanne walioingia fainali na kumkabidhi tuzo maalum mmoja kati yao aliyewazidi wenzake alioingia nao fainali.
Washiriki walioingia fainali ni Pr. Anna Tibaijuka, Dk. Asha-Rose Migiro, Anna Kilango Malecela na Dk. Maria Kham.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )
Post a Comment