SNURA AHAIDI KUPUNGUZA VIUNO VYAKE KWENYE VIDEO ZAKE MPYA BAADA KUAMBIWA KAKOSA MAADILI....NANI ALIMWAMBIA..?SOMA HAPA ...

Thursday, March 27, 20140 comments

Muimbaji wa ‘Nimevurugwa’ Snura amesema tangu video yake ya ‘Nimevurugwa’ ifungiwe kuchezwa kwenye TV na iondolewe kwenye mchakato wa tuzo za KTMA 2014, amejirekebisha kwa kiasi kikubwa.
Snura na Dance wake  ndani ya uwanja wa Yambone Mtwara.
“Tayari mimi nimeshabadilika kabla hata hatujafika huku kwenye Kili, sababu ilifungikiwa muda kidogo kabla mambo ya Kili hayajaingia na wimbo wangu wa ‘Ushaharibu’ nilikuwa nimeshafanya video pia, kwahiyo ukitoka watu watajua ni jinsi gani nimeweza kubadilika,” Snura amekiambia kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Times FM Alhamis hii.
“Wakati nafanya video ya Nimevurugwa sikuhisi kama ningefungiwa na kama ningejua naweza kufungiwa nisingekatika. Kitendo cha mimi kufungiwa kimenishtua kidogo na nisingependa niende tofauti na BASATA ningependa niende nao sawa, kwahiyo nilichokifanya kwenye wimbo wangu wa Ushaharibu, nimekatika ndio lakini hakuna viuno kama ambavyo vipo kwenye Nimevurugwa.”
Snura amewaomba radhi mashabiki wake wanaopenda viuno kuwa katika video zake zijazo hawataviona kama kwenye video zilizopita lakini wataendelea kuviona akitumbuiza jukwaani. “Na hii nafanya kwasababu tu natafuta riziki si kwamba nafanya hivi labda napenda sana kuonesha kiuno change stejini,” alisema na kuongeza kuwa mashabiki wake huchukua pale anapotumbuiza bila kuwapa viuno.
“Mimi ni mfanyabiashara, sina jinsi inabidi nimridhishe mteja wangu ili waweze kujaa kwenye show, ili waweze kunikubali nipate riziki, mimi natafuta riziki.”
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved