MWENYEKITI wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ amesema watafanya shindano la kumsaka mlimbwende wa kundi lao, siku ya sherehe ya kuadhimisha miaka mitatu ya klabu hiyo ambayo itafanyika Machi 28, mwaka huu.
“Hatuna vigezo vingi, nidhamu, urembo na kipaji halisi cha kucheza sinema. Msichana huyo ndiye atakayeibuka kidedea. Tunawaamini majaji wetu, watafanya kazi nzuri kuhakikisha tunampata Miss Bongo Muvi. Kila mwaka taji litakwenda kwa mrembo mwingine,” alisema Nyerere.
Post a Comment