"CHUNA BUZ CAFE"HUU NDIO MGAHAWA WA SHILOLE UNAVYO ITWA

Tuesday, March 18, 20140 comments

Zuwena Mohamed aka ‘Shilole’ amesema anatarajia kufungua mgahawa wake wa chakula maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Shilole
Akizungumza kwenye 255 ya XXL, Clouds FM leo,Shilole amesema ameamua kufungua mgahawa kwakuwa ana taaluma ya Hotel Management na pia mama yake alikuwa mama Ntilie.
“Mgahawa wangu ambao natarajia kuufungua hivi karibuni utakuwa naeneo ya Mwananyamala nyumbani ambapo nakaa mimi. Mgahawa utakuwa una vitu vingi za kisasa, kwaiyo chakula kitakuwepo kuanzia mchana mpaka asubuhi yaani. Hii sehemu itaitwa ‘Chuna Buzi CafĂ©’ ni jina ambalo nimeamua kuipa kwakuwa ni jina la nyimbo yangu. Kila kitu kipo ni bado tu kufungua.Mimi napenda sana kupika kwasababu mama yangu alikuwa mama Ntilie mkubwa sana na mimi mwanae kwasababu napenda biashara ya vyakula,mimi mwenyewe nimeshasomea Hotel Management kwahiyo najua na najua thamani ya chakula. Kwahiyo mtu ataacha kuvaa lakini atakula chakula, nimefanya kazi ya hoteli, Peacock Hotel, baadaye nikaja nikafanya Florida nikaja kuacha baada ya kupata pesa za biashara,” alisema.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved