Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limeziondoa nyimbo tatu kwenye mchakato wa tuzo za muziki Tanzania, KTMA kwa madai kuwa zinakiuka maadili ya Kitanzania. Nyimbo hizo ni pamoja na ‘Nimevurugwa’ wa Snura, ‘Uzuri wako’ wa Jux na ‘Tema Mate’ wa Madee.
Akizungumza nasi leo baada ya kupata taarifa ya kuondolewa wimbo
wake kwenye tuzo hizo, Madee amesema hajapendezwa na hatua hiyo.
“Sichukui hatua yoyote ila nawashangaa tu hao viongozi ambao
wanahusika na mchakato mzima. Sisi tunaandika nyimbo ambazo vijana wetu
wanazipenda,kwahiyo kama wameamua hivyo basi wawe wanatuandikia wao
nyimbo,kwasasabu sisi tunawaandikia vijana wenzetu, sasa unakuta hao
wanaoendesha mchakato ni wazee hawawezi kuchanganua maneno yetu,ifike
time sasa wawe wanatuandikia mashairi,” amesema Madee.
Post a Comment