Ni msanii ambaye anaweza kuwa ametajwa zaidi kwenye tuzo za KTMA 2014 lakini Diamond Platnumz hajaliacha Baraza la Sanaa Tanzania likae kwa amani kwa uonevu ilioufanya kwa Jux, Madee na Snura kutokana na kuziondoa nyimbo zao kwenye mchakato wa KTMA 2014.
Kupitia Instagram, Diamond ameandika:
"Ikiwa kweli tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na
vizazi vyetu pendwa, nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo
za kutoka nje, kuliko kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu
wake Haufikii hata robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele
toka nje…
"Hii ni sawa na kuzidi kuukuza mziki wa nje huku tukiudidimiza
na kuua mziki wetu… Will the target of reaching our goals ever be
achieved?? #Ni_Mtazamo_tu."
Post a Comment