Akizungumza na Kipindi cha Action & Cut cha Channel Ten hivi karibuni, Dokii alisema kutokana na jinsi alivyoshiriki katika kampeni mbalimbali za Kikwete hadi kupata ajali na kuumia mkono, wambeya wamekuwa wakimzushia kuwa alijipendekeza na hakupewa msaada wowote alipoumia.
“Nawashangaa wanaosema kuwa najipendekeza kwa JK, eti wanasema nilitelekezwa. Kwa taarifa yao tu ni kwamba, JK aliposikia nimepata ajali, alituma madaktari Wazungu kuja kunihudumia.
“Halafu hata wakisema najipendekeza pia naweza nikakubali, nisipojipendekeza kwake wanataka nikajipendekeze kwa nani? Najua hata wao wanatamani kuwa karibu na viongozi kama mimi,” alisema Dokii. .