AIBU:KIJANA AUZA PICHA ZA UTUPU ZA MAMA YAKE KWENYE INTERNET ILI AJIPATIE KIPATO

Thursday, October 17, 20130 comments


Kijana mmoja wa nchini New Zealand amefanya kitendo ambacho kimewastaajabisha watu wengi pale alipochukua picha za uchi za mama yake na kujaribu kuziuza kwenye internet ili apate pesa za haraka haraka. Wakati vijana wengi wenye umri wa miaka 18 wasingejaribu hata kupitisha mawazo ya mama zao wakiwa watupu wanakuwaje, hali ni tofauti kwa kijana Michael, mwanafunzi katika mji wa Auckland, New Zealand kwani yeye alichukua picha za utupu za mama yake Jennifer mwenye umri wa miaka 44 na kujaribu kuziuza kwenye internet.

Kwa mara ya kwanza alizipiga mnada picha tano za mama yake kwenye internet akizipa jina "Picha tano za uchi za mama yangu" ili kumkasirisha mama yake baada ya kurumbana naye, alisema kijana huyo bila aibu wakati akihojiwa na gazeti la Herald Sunday. Wakati tovuti ya TradeMe ilipozishtukia picha hizo na kuziondoa siku moja baada ya kuziweka, kijana huyo aliweka picha zingine za mama yake akizipa jina "Picha za mrembo" safari hii akiwa amepewa ruksa na mama yake huyo. Safari hii picha alizoziweka nyingi zilimwonyesha mama yake akiwa amevaa vizuri isipokuwa picha moja ambayo mama yake alikuwa amevaa kichupi tu. Michael ambaye hakutaka jina lake la pili litajwe alisema kuwa aliuza picha za utupu za mama yake ili apate pesa za 'chap chap'. Mama yake akiongea na gazeti hilo alisema kuwa alikasirishwa sana na picha za awali lakini alifurahishwa na picha za mara ya pili kwani alikuwa akionekana mrembo kweli na watu wengi walitoa maoni ya kumsifia. "Nilitaka asilimia 50 ya mauzo ya picha hizo" alisema mama huyo naye bila aibu na kuongeza " nitayakumbuka maoni mazuri yaliyotolewa juu ya picha zangu". Mama huyo alidai picha za mara ya pili ambazo mwanae alijaribu kuziuza zilipigwa na rafiki wa familia hiyo miaka michache iliyopita. Picha hizo ziliangaliwa mara 11,000 kabla ya kuondolewa na wamiliki wa tovuti hiyo kwa kuonekana hazifundishi jamii maadili mema.
"Hatutaki tovuti yetu iwe ndio sehemu ya watu kuweka picha za mama zao wakiwa na vichupi tu" alisema msemaji wa TradeMe

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved