MSANII WA MAIGIZO APATA HOMA BAADA YA KUZURU KABURI LA SAJUKI

Thursday, October 17, 20130 comments


MWIGIZAJI wa kitambo, Vanitha Omary amejikuta akipata homa kutwa nzima baada ya kuzuru kaburi la Juma Kilowoko ‘Sajuki’ maeneo ya Kisutu, jijini Dar.
Akizungumza na Amani, Vanitha alisema kuwa kila inapokaribia Sikukuu ya Idd El Hajj, Waislamu wana desturi ya kutembelea makaburi hivyo, alipofika makaburini hapo akiwa na ndugu zake ndipo alipata homa kutwa nzima.
“Tulimuombea na kufagilia kaburi lake na baada ya kumaliza nilianza kujisikia vibaya sana nahisi ni kutokana na kuwakumbuka marehemu wote waliotangulia mbele ya haki,” alisema Vanitha.
 
-Gpl
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved