Davido wa Nigeria kumwaga "burudani ya nguvu" katika fainali za Serengeti Fiesta jijini Dar wiki ijayo

Friday, October 18, 20130 comments



Homa ya tukio kubwa la burudani ambalo hufanyika kila mwaka inazidi kupanda, of course naizungumzia Serengeti Fiesta 2013 ambayo baada ya kuzunguka mikoani na kuacha historia sasa mashambulizi yamehamia katika fainali inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo jijini Dar es salaam.
 
Kila mmoja bado anajitahidi kubashiri ni wasanii gani wa kimataifa watakaoshambulia jukwaa hilo mwaka huu, lakini mmoja wao amewekwa hadharani jana (October 17) kupitia XXL ya Clouds FM naye si mwingine bali ni Dami Duro hit maker Davido.
 
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Davido kuperform Tanzania katika jukwaa la Fiesta hivyo inatoa picha ni kiasi gani patakuwa hapatoshi pale viwanja vya Leaders Jumamosi ijayo (Oct 26) katika fainali ya Serengeti Fiesta 2013.
 
Davido  ni  nani?
Jina lake kamili ni David Adedeji Adeleke aka Davido kutoka Nigeria. Ni mmoja kati ya wasanii wakubwa wa Africa na anatokea katika familia ya mfanya biashara bilionea aitwaye Dr Deji Adelek.

Davido ambaye mwezi November atatizmiza miaka 21 alizaliwa Atlanta, Georgia Marekani Novemba 21, 1992 na kukulia Lagos, Nigeria.
 
Alianza kuonekana kwenye spotlight mwaka 2011 kupitia wimbo wake maarufu ‘Back When’ aliomshirikisha star mwingine wa Nigeria Naeto C.
 
Mbali na kuimba Davido pia ni mwandishi wa nyimbo na producer na anamiliki Record label yake inayoitwa HKN Music.
 
Mbali na muziki Davido pia ni mwanafunzi wa chuo cha Babcock huko Nigeria akichukua Business Administration.
Kati ya Hit Songs za Davido ambazo bila shaka ataziperform live katika Serengeti Fiesta Jumamosi ijayo ni pamoja na Dami Duro, Back when, Gobe, na Zingine
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved