Jokate Mwegelo afunguka: Anasema hajafanya mapenzi kwa muda wa mwaka mmoja , Yupo SINGLE na anatongozwa na mamia ya wanaume kwa siku

Friday, October 18, 20130 comments



Hii  ni  mara  ya  kwanza  kwa  Jokate  Mwegelo  kuongelea  mambo  ya  chumban...

Maongezi  hayo  yalifanyika  kati  yake  na   Millard  Ayo   ambaye  ni  mtangazaji   wa  Clouds  FM.Katika  maongezi  hayo, Jokate  naye ameeleza  jinsi  anavyosumbuliwa  kutongozwa  na  mamia  ya  wanaume  kwa  siku 

Yafuatayo ni maongezi  yao: 

Millard Ayo: Nini kimekufanya ufunguke na hizi info ambazo hujawahi kuzizungumzia na mara nyingi umekua ukigoma kuziongelea kwenye media?

Jokate: Nahisi kwa sababu watu wanazidi kuizungumzia na wanaizungumzia sivyo, hawazungumzii kiuhalisia na kiukweli inanisumbua ndio maana nimeamua kusema kitu kidogo alafu niufunge huu ukurasa.
 
Millard Ayo: Imekua ikikusumbua kwa mda gani?
Jokate: Kwa muda mrefu, toka mwaka jana… kwenye facebook watu wanatoa comment na najua kabisa watu hawajaelewa hili swala na mimi sipendi mashabiki wangu kutokunielewa.

Millard Ayo:  umewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond pamoja na Hasheem?
Jokate: Hahahahahhaha !!!! Yeah..
 
Millard Ayo: Uhusiano wa nani kati ya hawa wawili ulidumu kwa muda mrefu?
Jokate: Wa Hasheem.. karibia miaka miwili mitatu
 
Millard Ayo: Na wa Diamond?
Jokate: Oooh kipindi kifupi sanaaa, sijui mwezi sijui miezi miwili… kidogo alinipa tabu, ila kiukweli nilitaka tu kwa sababu kuna watu wengi walikua wanasema Jokate yani vurugu, unajua sio kila kitu unachokisikia ndio chenyewe na media saa nyingine inapenda kuandika vitu ambavyo sio vya ukweli au wanaviwasilisha sivyo.
 
Millard Ayo: Sasa hivi uko single?
Jokate: Yeah, kwa muda mrefu tu niko mwenyewe alafu saa nyingine wananisumbua sana  tena  wengi  tu, lakini nafurahia kwa sababu naweza kufocus kwenye kazi zangu mfano wiki ijayo nakwenda kushoot movie na JB, muziki na biashara zangu kwa hiyo inanipa fursa nzuri kufanya vitu vyangu, yani mwenyewe kujiamulia asubuhi nakwenda kufanya vitu vyangu hivyo bila kusumbuliwa si unajua Wanaume wanaweza kusema wanataka attention nini… sio kitu kibaya atleast kwa sasa hivi.
 
Millard Ayo: Umekaa single kwa muda gani sasa hivi? zaidi ya mwaka?
Jokate: Yeah, kwa zaidi ya mwaka mmoja sijafanya  mapenzi… sijawa na mtu ambae nimeweza kumuita like oohh this is my boyfriend… najua ni ngumu lakini nabusubusu watu wengi…. hahah a hah natania hapo, basi tu imetokea hivyo pengine bado sijapata mtu ambae nimeona ataweza kuwa kama wale..
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved