Mzee Mjuto
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni akijiandaa kwenda nchini Uturuki kikazi, Mzee Majuto amedai kuwa hakuna mchekeshaji ambaye anaweza akashindana naye zaidi ya Mr. Bean.
“Mimi Nigeria naona kuna watu wa kawaida sana,labda nishindane na kama Mr Bean hivi,ndio nitajitaidi nimpiku, sitakubali anipiku na hiyo ndio sanaa. Umri unaenda kama kule India kuna Amitabh Bachchan na wengine wengi nawafahamu katika filamu, kwahiyo ni juhudi sema wenzetu ni wazungu na walianza mapema, sasa hivi tumepata shavu la safari ya Uturuki itatuanzishia safari nyingine za kazi,” alisema.
Pia Majuto amesema kuwa kwa upande wa Tanzania sanaa yake ni kubwa na inamuendeshea maisha yake vizuri.
“Mambo yangu sio mabaya kwa hapa nyumbani,Mungu anasaidia kwa kazi ambazo nafanya sokoni zinafanya vizuri,nina nyumba,magari na nimefanikiwa kujenga Msikiti kupatapahala pa kuswalia si unaona uzee huu.”
Post a Comment