Hii
ni taarifa kutoka Kenya ambapo inasemekana Wazazi katika kaunti ya
Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya
mwalimu mmoja kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi kupoteza
maisha.
Mtoto huyo
inasemekana alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai na alipokua
akipelekwa hospitali alifariki dunia,ambapo wazazi hao wameandamana kwa
amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
Polisi
nchini Kenya wamemtia mbaroni tayari mwalimu huyo na kwa sasa
anashirikiwa na Polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanywa,Mtoto
huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi iitwayo
Roka Preparatory.
Wengi wa wazazi wenye watoto
wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine ambapo Nchi
ya Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu
miaka kumi iliyopita na hii ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu
vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.
Source:Bbc Swahili
Post a Comment