Watu
watatu waliofahamika kwa majina ya Msagala, Jacob na Mhando wakazi wa
Bunju jijini Dar es Salaam mchana huu wamefariki dunia.
WATU watatu waliofahamika kwa majina ya Msagala, Jacob na Mhando
wakazi wa Bunju jijini Dar es Salaam mchana huu wamefariki dunia baada
ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto kwenye machimbo ya
Mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliyefahamika kwa jina la Kara Arjan
yaliyopo Bunju-Mbweni jijini.Habari zilizopatikana eneo la tukio zilisema kuwa machimbo hayo yalishapigwa marufuku kutokana na watendaji wake kufanya kazi katika mazingira hatarishi. Wachimbaji hao wakiwa kazini, sehemu ya machimbo hayo iliporomoka na kuwafukia.
(PICHA/HABARI : RICHARD BUKOS / GPL 0713 562001)
Post a Comment