NDEGE ILIOPOTEA YAKUTWA BAHARI YA HINDI..SOMA ZAIDI

Monday, March 24, 20140 comments


Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak akitangaza leo juu ya utafiti wa rada kuonyesha kuwa ndege iliyopotea imeangukia katika bahari ya Hindi.
Tangazo hilo limetolewa wakati ndege ya majini ya Australia ikiwa njiani kuelekea kunakoonekana vitu hivyo vilivyoonwa na ndege za kijeshi wakati wa msako wake.
Wanajeshi wa jeshi la Australia wakiwa ndani ya ndege katika kituo cha Kijeshi cha AP-3C Orion.
WAZIRI Mkuu wa Malaysia, Najib Razak ametangaza habari mpya kwamba ndege ya abiria iliyopotea ilimalizia safari yake kusini mwa bahari ya Hindi, tangazo ambalo limewavunja moyo wanandugu wa abiria.
Ndege hiyo ya abiria ya Malaysia iliyokuwa na namba MH370 ilitoweka katika rada za kiraia saa moja baada ya kuruka kutoka Kuala Lumpur kuelekea  Beijing ikiwa na watu 239 ndani yake hapo Machi 8 mwaka huu.
Hakuna habari zilizothibitishwa juu ya kuonekana kwa mabaki ya ndege hiyo, ingawa kumekuwa na vitu vinavyoonekana huko pwani ya Australia vinavyodhaniwa huenda ni sehemu ya chombo hicho. Ndugu wa abiria waliokuwemo ndani, wameanza mipango ya kusafiri kuelekea huko.
Hata hivyo, vitu vilivyoonekana kwenye satellite ya China na Ufaransa, bado havijaweza kufikiwa na kutambuliwa kama vina uhusiano wowote na ndege hiyo ambayo ni gumzo kwa sasa duniani.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved