BABA RAIS,MTOTO MBUNGE,MAMA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CHAMA,WACHAMBUZI WA MAMBO WAMFANANISHA RAISI KUKWETE NA MUSEVEN WA UGANDA

Sunday, March 16, 20140 comments


RAIS Jakaya Kikwete Ameeanza kumuiga Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa kile kinachodaiwa ameanza kurithisha uongozi Famili ya yake ndani ya Chama cha Mapinduz CCMi ,.
   Haya yamegundulika Baada ya Mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete Kupitishwa na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapindzu CCM, yaani NEC kugombania Ubunge wa Katika Jimbo la Chalinze.

Kupitishwa kwa Ridhiwani na NEC, imekuja ikiwa Tayari Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho ambapo alichaguliwa Kupitia Wilaya ya Lindi Mjini
Huku naye Mtoto wake wa kiume Ridhiwani ni Mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Bagamoyo .Ikumbukwe wote hao walipita bila kupingwa.

Duru za kisiasa zinasema Rais Kikwete ameanza kumiga Rais Musevini kutokana Rais huyo wa Uganda kwenye utawala wake amewaweka Ndugu zake kwenye Nafasi za juu za Jeshi la Uganda hadi kwenye utawala Wa serikali.

Museveni,ambaye aliweka Rekodi Barani Afrika kwa kitendo cha kumteua Mkewe kuwa Waziri wa Masuala ya Karamoja Nchini humo,bali pia amegawa madaraka ya umma kwa ndugu zake wa Kuzaliwa.
Mdogo wake,Salim Saleh,kuwa mshauri Mwandamizi wa Rais akiwa amemuhamishia kutoka Waziri wa Fedha wa Uganda.Mwanae wa Kumzaa Bregedia Muhoozi ni mkuu wa Vikosi maalum vinavyomlinda Museveni.
Duru hizo zinasema licha ya kuwa tofauti na anavyoanza Rais Kikwete,lakini Rais Kikwete ameweka Rekodi ambazo azikufikiwa na Watangulizi wake kwa kitendo chake cha kuidumbukiza Familiya yake kwenye Siasa.

Wachambuzi Mbalimbali waliozungumzia hili,akiwemo Mwandishi na Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Tanzania Daima Edsoni Kamukara katika moja ya Makala yake alishangaa kwa hatua taifa letu inayofikia ya Viongozi Kuanza kupandikisha viongozi watoto wao kwenye Utawala huku wakiwa hawana uwezo.
“Tutakuja kujikuta siku moja tuna serikali inayoundwa na ‘family friends’. Ni kweli inatokea sehemu nyingi duniani ambako watoto wanawarithi wazee wao. Lakini karibu mara zote ukifuatilia tabia hiyo ya serikali za ‘kifamilia’ utakuta uporaji au matumizi mabaya ya mali za umma.

Ikumbukwe kwamba jimbo analotaka kugombea Ridhiwani ni jimbo ambalo baba yake pia alikuwa mbunge kabla ya kupaa hadi kuwa rais. Uteuzi huu hata kama ulifuata vigezo vya wagombea unaweza kufanya watu wakaanza kujiuliza tena ile tambo maarufu ya Chama Cha Mapinduzi kwamba CCM ina wenyewe! Je, wenyewe ndio baba na watoto wao au inahusisha pia kila aliye na kadi ya chama hicho?ilisema makala hiyo ya Kamukala.
Ridhiwani kikwete alikaliliwa na Vyombo vya Habari wiki hii alisema jina la Kikwete alina mashiko yoyote kwake katika kushinda ujumbe kwenye baraza kuu la vijana la CCM,pia alina mvuto kupata U_NEC na hata sasa nafasi ya yeye kugombania ubunge wa chalinze.

Duru za Kisiasa zilipinga kauli hiyo ya Mtoto wa Rais kikwete mwenye miaka 30-40 na kusema yeye ni mtu anayeangalia jua angani mchana saa sita wakati jua kali na kusema kwanini jua alingai.

Yeye anatamka hivyo amekuwa kipofu asiyejua chochote kinachoendelea,Ridhiwani anatoa kauli hiyo akiaamini kila mtanzania ni Juha na hajui kupambuna mambo,Jina la Baba yake Tangu anakuwa Waziri mpaka leo Rais wa Nchi haijaweza kumsaidia mpaka yeye kufika hapo.
Udhaifu mkubwa wa Mtoto huyo wa Rais kujenga hoja,anaonyesha Taswira moja kwamba kijana huyo asemi ukweli na anajitahidi kusema uongo kwa nguvu sana ili kubadilisha uongo kuwa ukweli,ukweli ni Kwamba kikwete Ndiyo gia yake kubwa la kufanikiwa. 



Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved