TUKIO LA UVAMIZI FEKI WA ALI-SHABAAB LAIKUMBA MWANZA NDANI YA HOTELI YA GOLD CREST...WANANCHI WAPAGAWA NA KUILILIA SERIKALI...

Saturday, November 9, 20130 comments


Wakazi wa jiji la Mwanza juzi  majira ya saa 4 asubuhi waliwekwa njia panda na kujawa hofu kubwa kufuatia vikosi vya askari kanzu, FFU, askari polisi na zimamoto wakiwa na vifaa sambamba na magari yao walipolivamia jengo la Hotel Gold Crest na kuanza saka saka za kujiweka sawa huku wakiendeleza mapambano na jamaa ambao walijipanga mithili ya wahalifu.

Hali hiyo ilisababisha magari pikipiki kusimama kwa muda huku wananchi wakiingiwa hofu na woga, wengine wakikimbia na baadhi ya wafanyabiashara walifunga maduka yao wakifananisha na lile la Westgate la jijini Nairobi nchini Kenya..
 
Hata hivyo mpaka zoezi hilo linamalizika hakuna mwananchi aliyeweza kubaini kuwa tukio hilo lilikuwa ni la uigizaji, kila mmoja alikuwa akisimulia kivyake sekeseke zima, lakini mapango mzima ulikuwa ni kuvinoa vikosi vya polisi na Zimamoto juu ya kukabiliana na uhalifu kwenye majengo makubwa ya huduma mbalimbali.  



Wateja wa kituo cha mafuta kilichopo karibu na hotel Gold Crest jengo ambalo ndiko zoezi lilikuwa likifanyika pamoja na wateja wa ofisi za PPF, duka la Vodacom Mwanza na Benki ya NMB zilizopo katika jengo hilo walikosa huduma kwa muda huku wengine wakitimka maeneo hayo kwa tahadhari wakidhani ni live.




Watu wakihaha nao polisi wakiweka ulinzi mkali eneo la tukio. 


Harakati zikiendelea eneo la tukio.
Polisi wakiwaweka chini ya ulinzi 'wahalifu bandia' katika zoezi lililozua taharuki kwa kwakazi wa jiji laMwanza.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved