MTOTO Khalidi Juma mwenye umri wa miaka minne, mkazi wa Vingunguti
jijini Dar es Salaam, yuko katika mateso makali baada ya jicho lake moja
kutolewa katika harakati za kumnusuru na ugonjwa wa Kansa, huku lingine
nalo likilegea.
Akizungumza na mwandishi wetu, mama wa mtoto huyo Hadija Kilindo, alisema alimzaa mtoto huyo akiwa na afya njema, lakini alipofikisha umri wa miezi tisa ndipo alipogundua kitu cheupe kwenye mboni ya jicho lake.
Akizungumza na mwandishi wetu, mama wa mtoto huyo Hadija Kilindo, alisema alimzaa mtoto huyo akiwa na afya njema, lakini alipofikisha umri wa miezi tisa ndipo alipogundua kitu cheupe kwenye mboni ya jicho lake.
Baada ya hali hiyo, alisema alimpeleka katika hospitali inayotibu
watu wenye ulemavu mbalimbali ya CCBRT iliyopo Msasani jijini Dar,
ambako baada ya kupimwa, aliambiwa mwanaye alikuwa na kansa.
“Baada ya kuambiwa mtoto wangu ana ugonjwa wa kansa sikuwa na jinsi,
nilikubali afanyiwe upasuaji kwa ajili ya kuliondoa jicho hilo ili
kuokoa maisha yake,” alisema.
Mama huyo alisema ilipofika mwaka 2012, jicho lingine lilianza
kumuuma huku likiwa linavimba, lakini alipompeleka katika Hospitali ya
Muhimbili, aliambiwa kansa imeshaenea mpaka kwenye ubungo, hivyo arudi
naye nyumbani kwani hawezi kuishi kwa muda mrefu.
“Kwa kweli nilivyoambiwa hivyo nilinyong’onyea mwili mzima nikawa
sina jinsi kabisa na nikapoteza matumaini kabisa ya mwanangu kuendelea
kuishi tena,”alisema.
Alisema alirudi nyumbani huku maumivu ya kijana wake yakiendelea na
mwishoni, jicho lake likawa halioni tena. Kuhusu jicho lililotolewa,
mama huyo alisema alikuwa akilitoa na kulirudisha kwa ajili ya
kulisafisha, lakini hivi sasa hawezi kulitoa tena kwa vile kuna nyama
zilizolishika na hivyo kumsababishia maumivu makali mno mwanaye hasa
kichwani.
“Unavyotuona hapa usiku hatulali kabisa, mtoto ni kulia kwa maumivu,
amefikia wakati hawezi kula vizuri na anatumia muda mwingi kulia,”
alisema.
Mama huyo aliongeza kueleza kuwa kutokana na hali ya mwanaye, anakosa
muda wa kufanya chochote cha kujiingizi kipato, hivyo kuwa katika
wakati mgumu mno kimaisha, hasa kwa vile baba mzazi wa mtoto huyo
alimkimbia tokea alivyoanza kuumwa.
“Mimi naamini kabisa labda
nikipata msaada nikienda hata kwa wachina nitapata hata dawa ya
kumpunguzia mtoto wangu maumivu anayoyapata kwa hivi sasa,” alisema.
Post a Comment