MUME AMKATA MKEWE MKONO KISA WIVU WA MAPENZI...

Friday, October 18, 20130 comments

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Nyamikoma Kata ya Bugarama Wilaya ya Geita, Leah Clement (24), anadaiwa kukatwa mkono wake wa kushoto na mumewe kutokana na wivu wa mapenzi.

Hivi sasa mwanamke huyo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita akiendelea kupatiwa matibabu. Aidha, mtuhumiwa wa ukatili huo, anadaiwa ametoroka na kwenda kujichimbia kwa `sangoma' kwa imani kwamba hatakamatwa.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 9, mwaka huu saa
1:30  usiku katika kijiji cha Chifufu kata ya Bugarama wilayani Geita.
Imeelezwa kwamba 
mtuhumiwa huyo alikwenda jikoni kwa mkewe na kukuta akisonga ugali kisha akamvamia na kumshambulia kwa panga lengo likiwa ni kumkata shingo yake. 

Hata hivyo, mkewe aliwahi kujikinga shingoni kwa kutumia mkono wake wa kushoto na hivyo kusababisha ukatwe.

Akizungumza akiwa katika wodi alikolazwa majeruhi huyo, Mkuu wa Wilaya ya Geita,
Manzie Mangochie, aliapa kuwa vitendo vya aina hiyo haviwezi kuvumiliwa
katika ya jamii kwani licha ya kuwa vya unyanyasaiji wa kijinsia, pia
vinakiuka haki za binadamu na sheria za nchi.
Mangochie ameagiza mtuhumiwa huyo, Mussa Lutobeka (34), akamatwe mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kadhalika, ameagiza mganga wa kienyeji anakodaiwa kukutwa mtuhumiwa amehifadhiwa, pia akamatwe.
Ofisa
Mtendaji wa kata ya Bugarama, Juma Choma, alisema walimkamata mtuhumiwa
huyo nyumbani kwa mganga wa kienyeji, Mashindeke Mwanzalima (47), akiwa
amejificha chini ya uvungu wa kitanda.
Hata hivyo, Choma alisema walipokwenda nyumbani kwa mganga huyo wa kienyeji, alikana kuwapo kwa mtuhumiwa huyo.
Lakini
alisema baada ya kumbana na kuipekua nyumba yake, walimkuta mtuhumiwa
wa ukatili huo akiwa amejificha uvunguni mwa kitanda.
"Ndipo nilipoamuru mganga huyo naye akamatwe," alisema.

Watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Leonard Paul, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na watuhumiwa kukamatwa.
Akizungumzia
tukio hilo huku akibubujikwa machozi wodini likolazwa, Leah alisema
kabla ya tukio hilo, mumewe ambaye ana wake wawili, alikuwa akimtishia
kuwa siku moja atamuua kama hataondoka.
Mke mwingine wa mtuhumiwa huyo anadaiwa alikimbia.
Kutokana
na vitisho hivyo, Leah alikwenda kutoa taarifa kwenye ofisi ya kijiji,
lakini askari mgambo waliokwenda nyumbani, hawakumkuta mtuhumiwa baada
ya kutoroka.
Leah alisema alilazimika kuondoka nyumbani kwa mumewe na kwenda wa baba yake mdogo hadi ufumbuzi utakapopatikana.
Kwa
mujibu wa Leah, aliolewa na mume huyo mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka
19 baada ya wazazi wake kupokea mahari ya Sh. 400,000 kati ya 500,000
alizokuwa amepangiwa kutoa.
Aidha, alisema wazazi wake (Leah), Clement Jading'wa na Rehema Rehema Kasabuku, walitengaba tangu mwaka 1995.
Leah anasema wakiwa na mume wake, wamebahatika kupata watoto wawili, Happiness Mussa (5) na Merciana Mussa (3).
Hata hivyo, alisema watoto hao kwa sasa wanaishi kwa baba yake mzazi tangu walipofarakana na mumewe.
Daktari
wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dk. Leah Kusalula, alisema
ulemavu alioupata majeruhi huyo, ni wa kudumu na ni kitendo cha ukatili
wa kutisha wa kijinsia ambao haupaswi kuvumiliwa


Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved