Maelfu ya Wamarekani wamerejea makazini kufuatia Bunge la Congress la nchi hiyo kupitisha bajeti ya nchi hiyo baada ya siku 16 za kukwama na kusababisha serikali kufunga baadhi ya shughuli zake.
Akizungumza katika Ikulu ya nchi hiyo baada ya kusaini muswada huo, Rais Obama amesema hatimaye tishio lililoudhoofisha uchumi wa Marekani sasa limeondoka.
Makamu wa Rais wa nchi hiyo Joe Biden, aliwatembelea wafanyakazi wa serikali walioonyesha kufurahia hatua hiyo ya wanasiasa katika maeneo mbalimbali ya ofisi za serikali.
Baadhi ya wafanyakazi hao, wamewalaani baadhi ya wanasiasa wa nchi hiyo kwa kuweka mbele maslahi binafsi badala ya kujali umma wa Wamarekani.
Post a Comment