Akizungumza na mpekuzi wetu,Lulu alisema kwamba pamoja na kwamba wanaume wengi wa kila aina na wenye pesa nyingi wanamtongoza kila siku, lakini pia anafurahia kupendwa na kwamba anapogundua kwamba anapendwa huwa anajisikia raha na mwenye rufaha zaidi.
"Ninatongozwa sana kila siku na wanaume, tena wenye pesa zao.Binafsi nafurahi sana kupendwa na ninapogundua kwamba mtu flani ananipenda huwa najisikia faraja sana..
"Kutongozwa kwa mwanamke yeyote mzuri ni jambo la kawaida.Kukubali au kukataa ombi la mwanaume ni maamuzi ya mtu binafsi. Mpekuzi naomba usiniulize ni wangapi nimewakubali au kuwakataa
( huku akicheka )
Akifunguka zaidi kuhusu bahati hiyo , Lulu alidai kuwa hali ya kutongozwa sana iliongezeka baada ya yeye kutoka gerezani...
"Niliporejea uraiani, kasi ya kutongozwa ilizidi sana tofauti na nilivyokuwa nadhani".