INATISHA..MUME AMPIGA MKEWE NA CHUMA NA KUMWAGIA TINDIKALI MPAKA KUFA..

Wednesday, October 16, 20130 comments


 
Jeshi la polisi Nchini Nigeria linamtafuta mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jila la Sunday Eze(33) kwa kosa la kumuua mkewe na kisha kukimbilia kusiko julikana.

Siku ya ijumaa october 11 Sunday Eze kutoka  Obiofia Nnewichi Nnewi katika Jimbo la Anambra,Alikwenda nyumbani kwa baba mkwe wake huko Edoji Uruagu kumuona mke wake ambae warikuwa wametengana kutokana na kutofautiana katika maamuzi yao.

Akielezea mkasa huo baba wa mwanamke (baba mkwe) alisema kuwa Sunday alikuja nyumbani kwake siku ya ijumaa na kudai kuwa amenunua kiwanja kipya kwa hiyo amekuja kumchukua mkewe aende akamwonyeshe kiwanja hicho lakini mwanangu alikataa ikabidi Sunday atumie muda mwingi kumshawishi ndipo alipokubali na kisha kuondoka nae.

Walipokaribia katika Serikali ya Mtaa huko Ekwusigo, Sunday Eze alimgeuka mkewe na kuanza kushambulia alimpiga na chuma na kisha  kummwagia tindikali mwilini.

kama vile haitoshi baada ya kipigo hicho Sunday Eze alichukua kiasi cha tindikali kilichokuwa kimebakia na kisha kumnywesha mkwe kwa lazima, Ndipo mwanamke huyo alipopiga mayowe ambapo polisi waliokuwa wanapita karibu na eneo hilo walifika mara moja na kukuta mwanamke huyo akiria kwa uchungu huku mumewe akiwa kasha kimbia muda mrefu.



Polisi walimchukua mwanamke huyo na  kumkimbiza katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha  Nnewi iitwayo "Nnamdi Azikiwe" lakini kwa bahati mbaya mwanamke huyo alipofikishwa hospitalini hapo alifariki dunia.
Kwa mujibu wa baba mkwe anadai baada ya kufanya unyama huo Sunday aliwaita wanafamilia siku ya tar 13 october kwa lengo la kutaka kukutana nao na kuwaomba msamaha kwa kitendo alicho fanya lakini hakutaka kusema ni kwa nini alimfanyia unyama huo mkewe
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved