DIAMOND, YAMOTO BAND KUTUMBUIZA SIKU YA MSANII DAR

Thursday, October 23, 20140 comments


Msanii Diamond (mwenye shati nyeupe) akiwa na Yamoto Band.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
WANAMUZIKI Diamond na  Yamoto Band wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Siku ya Msanii litakalofanyika  Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo katika ukumbi wa Maelezo , Ofisa Uhusiano wa Siku ya Msanii (SYM) , Peter Mwendapole, amewataja wasanii wengine watakaokuwapo ni pamoja na mwanamitindo Asia Idarous, Miss Tanzania, Miss Universe na  wasanii toka Kenya, Erick na Fred Omondi huku mgeni rasmi  akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Gharib Bilal.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved