Baada ya tukio la Westgate ambalo lilichukua maisha ya watu wengi, jiji la Nairobi limekumbwa na tishio jingine la aina hiyo kwenye eneo la biashara la Nakumatt Junction Barabara ya Ngong ambapo yamekutwa masanduku manne ya kubebea risasi kwenye eneo la kuegesha magari kwenye vyumba vya chini (Basement).
Masanduku hayo yalipatikana ndani ya toroli la kubebea mzigo kutoka
kwenye duka la jumla la Nakumatt ambapo walioshuhudia wamesema sanduku
hizo zilikuwa zimeandikwa ‘explosion’ na walipoitwa wataalam wa mabomu
wakagundua kuwa sanduku ni za kubebea milimita 9 risasi za bunduki aina
ya ceska ama Mp5 machine gun.
Masanduku hayo yaligundulika wakati wafanyakazi wakirudisha matoroli
hayo ndani baada ya wateja kuyatumia na kuyaacha eneo la parking.
Post a Comment