
Hata hivyo, RadarOnline wamedai kuwa wawili hao watahudhuria harusi hiyo. Harusi yenyewe itakuwa na masharti kibao. Yeyote atakayehudhuria hatoruhusiwa kwenda na simu ya mkononi na atasaini fomu maalum.

Wapenzi hao hawataki kurudia kosa lilofanyika kwenye sherehe ya kuvishana pete bale mwanzilishi mwenza YouTube, Chad Hurley alipochukua video ya tukio na kuiweka Youtube. Kim na Kanye walimshtaki.

RadarOnline inadai Jay Z na Beyonce hawatoguswa na sharti hilo, wanaweza kuingia na simu zao.

“There is no way Kanye would ever even dare to ask Jay Z or Beyonce to sign a non-disclosure agreement, or take away their cellphones. He knows that neither one of them would betray his trust,” kilisema chanzo hicho.
Post a Comment