
Huu ni mtaro wa kupitisha maji taka ambao umepita katikati ya Hospitali ya Palestina ambapo ulifumuka na kusababisha kusambaa kwa maji machafu katika kila kona ya hospitali hiyo.
Mmoja wa wagonjwa akiwa anangojea kupata huduma baada ya mvua hiyo kubwa kuisha. 
Haya ni maji machafu ambayo yametapakaa kila sehemu ya hospitali. 
Kushoto
ni mgonjwa akiwa amelala juu ya benchi ambapo pembeni kuna maji na
matope ambayo yamechanganyikana na kinyesi kutoka katika vyoo mbalimbali
katika makazi ya watu. 
Hii ndio hali halisi ya chemba hii ambayo ipo ndani ya Hospitali ya Sinza Palestina. 
Hizi ni chemba zaidi ambazo zipo nje na pia zimeungana na zilizopo ndani ya hospital hiyo. 
Wagonjwa zaidi wakingojea waganga kufika pia kumalizia kusafishwa kwa vyumba hivyo ili wapate kuhudumiwa. 
Moja ya chumba ambacho kilikuwa kimejaa tope kikingojea kusafishwa. 
Hapa hata hapapitiki. 
Baadhi ya viti vikiwa vimeegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa usafi. 
Hakuna mtu katika maeneo haya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha. 
Kila kitu kimekaa hovyo hovyo baada ya mvua kubwa kunyesha.
Baadhi ya vifaa vya kutibia wagonjwa vikiwa juu ya moja ya kitanda cha kutibia wagonjwa. 
Huu
ndio mtaro wa maji machafu ambapo maji kutoka nje yamepita ndani ya
hospitali hiyo na kusababisha maafa baada ya mtaro huo kuziba.
****
Mapema
mchana wa leo kumetokea mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya Jijini
Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa baada ya maeneo mengi
kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara, nyumba za
watu pamoja na maeneo mbalimbali.
Mvua hizo kubwa ambazo hata mamlaka ya
hali ya hewa wametahadhalisha kwamba zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014
hadi Tarehe 7.03.2014 zimesababisha usumbufu mkubwa katika Hospitali
ya Halmashauri ya Kinondoni Sinza - Palestina kujaa maji kila kona na
kupelekea wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya meza na viti wakikwepa
maji hayo wakati wengine wakikimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.
Walikwepa maji hayo kutokana na kwamba si
ya mvua tu lakini yalikuwa ni machafu yaliyochanganyikana na maji
kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo.
Baada ya mvua hiyo kuisha iliwalazimu wafanya usafi wachukue muda wa
zaidi ya dakika 30 kufanya usafi na kutoa matope yaliyokuwa yamejaa kila
chumba.
Akiongea kwa simu Mganga Mkuu wa Hospitalu hiyo amekili kwamba kuna usumbufu mkubwa wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa kiasi kikubwa.
Ameongeza kwa kusema kwamba kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
Nao baadhi ya wagonjwa ambao wengine walikuwa katika hali ambayo si nzuri wamesema wanaiomba serikali itazame tatizo hilo maana licha ya maji hayo kuwa mengi lakini pia ni hatari kwa afya zao kwa ujumla.
(Picha zote na Dar es salaam yetu)
Post a Comment