Kupitia picha zilizotolewa na huduma hiyo kupitia ukurasa wake wa
facebook, umeonyesha waumini wakikimbilia matawi ya miti na kuanza kula
majani yake, huku mmoja wa waumini aliyefika kanisani hapo kwa mara ya
kwanza amesema amepona jino lililokuwa likimuuma mara baada ya kula
majani, amesema kwamba alifika kanisani hapo kwa mara ya kwanza siku ya
ijumaa akiwa na dawa za kutuliza maumivu pamoja na panado lakini
hazikumsaidia ila majani yalimponya na kwamba akirudi nyumbani mumewe
(ambaye pia mtumishi) atafurahi sana kwa uponyaji huo.
Huduma hiyo ambayo inaongozwa na mtume msomi Lesego Daniel imekuwa
ikipingwa na watu wengi hasa baada ya tukio la waumini kula nyasi huku
pia mtume huyo mda mwingine huwafanyia maombi waumini wake huku akiwa
amewakanyaga migongoni. Licha ya kelele kutoka kwa viongozi wa dini na
makanisa mbalimbali kuwakataza waumini wao na wakristo kuwa makini na
huduma ya mtumishi huyo, ndio kama wamewaruhusu kwenda huko kwakuwa
inasemekana huduma hiyo imeendelea kujikusanyia waumini kila kukicha.
Huduma hiyo ilikuwa ikifanya huduma zake katika majengo ya chuo kikuu
cha teknolojia cha Tshwane kwasasa wamepata enero lao ambalo wameliita
shamba la Rabboni ambalo wanatarajia kuhamia huko jumapili ijayo ya
tarehe 4.
Post a Comment