Na Mwandishi wetu,Geita yetu Blog
WIKI moja baada ya Tanzania kuungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha siku ya wanawake duniani,kauli mbiu ikiwa ni "chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia" mkoani Geita hali imekuwa tofauti baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Modester Shija (55-60) mkazi wa kitongoji cha Kamlale,kijiji cha Nyawilimilwa kata ya Kagu wilayani hapa kuuliwa kikatili kwa kukatwa mapanga Machi 14,mwaka huu na watu wasiojulikana.
WIKI moja baada ya Tanzania kuungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha siku ya wanawake duniani,kauli mbiu ikiwa ni "chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia" mkoani Geita hali imekuwa tofauti baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Modester Shija (55-60) mkazi wa kitongoji cha Kamlale,kijiji cha Nyawilimilwa kata ya Kagu wilayani hapa kuuliwa kikatili kwa kukatwa mapanga Machi 14,mwaka huu na watu wasiojulikana.
Imeelezwa kuwa Machi 14,majira ya saa 19:30 jioni Bi.Modester Shija akiwa jikoni anaandaa chakula cha usiku walifika wanaume wawili waliovalia makoti meusi mara baaada ya kukaribishwa mmoja wa wanaume hao aliomba maji ya kunywa mara baada ya kunywa maji aliingia jikoni alikokuwa mama huyo huku akisikika anauliza kwa kisukuma "mayo otale kubiisha? akimaanisha Hujaivisha? kabla ya kujibiwa ilisikika sauti ya kulalamika ya mwanamke " nimewakosea nini? wakati kijana mmoja anakwenda kuangalia ni kitu gani kinatokea nao naye akatishiwa panga ndipo akakimbia huku akipiga kelele za kuomba msaada.
Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha mmoja wa watoto wa marehemu Juma Chalula (23) alidai kuwa siku ya tukio majira ya saa moja na nusu jioni wakati anajiandaa kwenda kuoga baada ya kutoka shambani,walifika wageni wanaume wawili ambao hawatambui mara baada ya kuwakaribisha nje mmoja aliomba maji ya kunywa,alimfuatia jikoni,baada ya kumaliza kunywa maji alisema ngoja awasalimie jikoni,baada ya muda kidogo alisikia mama yake akipiga kelele wakati anaenda kumsaidia akathibitiwa na yule aliyekuwa amebaki nje baada ya kuchomoa panga.
"wale watu walivalia makoti meusi kumbe ndani walificha mapanga,mmoja aliniomba maji ya kunywa baada ya kumaliza akadai asalimie jikoni kumbe alikuwa anakwenda kumuua mama yangu,dakika aikuisha nikasikia mama anasema kwa sauti ya kulalamika akidai" nimewakosea nini jamani" wakati naenda kuangalia nikatishiwa na kukimbizwa na mmoja aliyekuwa amebaki nje,nilikimbia huku napiga yowe ila sikupata msaada wa haraka kutokana na nyumba zetu kuwa mbalimbali" alisimulia Juma Chalula mtoto wa marehemu.
"siku hiyo nilisikia saa moja jioni "mwamo" yaani yowe ila baada ya kufika kwenye tukio tulikuta wameshaondoka hao wauaji,kiukweli kwenye kitongoji changu ni tukio la kwanza na limetushtua sana,na kwa hali hii lazima tuwasake hao watu na tuwapate" alisema
Mwenyekiti wa kitongoji.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw.Mashauri Elisha alidai kuwa baada ya kusikia yowe aliwaongoza wananchi kuellekea eneo la tukio amba baada ya kufika walikuta tayari mama huyo akiwa ameuliwa kwa kukatwa panga shingoni na kwenye mabega yake huku mwili wake ukiwa umelala jikoni ndipo walipoanza kuwasaka wauaji hao ila hawakuwapata
Afisa mtendaji wa kijiji cha Nyawilimilwa Bw.Charles Kumalija alidai kuwa atahakikisha anasaidiana na polisi ili wauaji hao wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo husika,aliwataka wananchi kuwafichua waalifu wote ili sheria ichukue mkondo wake dhidi yao.
"yeyote anayefahamu hawa watu wanaojihusisha na vitendo hivi viovu alete taarifa ili wakamatwe la sivyo watatumaliza,haya matendo yanatutia aibu ni mambo ya kizamani tunatakiwa kubadilika" alisema Kumalija.
Jeshi la polisi wilayani Geita limethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kudai chanzo bado kinachunguzwa na kwamba linamshikilia Hamis Chalula (41)mkazi wa Kamlale kuhusiana na tukio hilo.
Post a Comment