WASANII WA BONGO MUVI WALIOWAI KUHATHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA WAHANIKWA HADHARANI PEUPE..WAONE MWENYEWE

Wednesday, March 26, 20140 comments


Msanii wa Bongo Flava maarufu kama Q Chief ni mmoja ya wasanii waliowahi kuweka wazi  na kukiri juu ya matumizi yake ya madawa ya kulevya,aliweza kujihusisha na matumizi ya madawa hayo hatari ya kulevya kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, jambo ambalo lilipelekea kushuka kwake katika ramani ya muziki.



Aliwahi kutesa na ngoma zake nyingi ikiwemo hit single yake iitwayo Zamani,Akiwa ni mmoja wa waasisi wa bongo fleva hapa Tzee, kwa kuweka mchango mkubwa wakufanya muziki wa bongo fleva upewe heshima yake.Baada ya kuingia katika janga hili la taifa kama ilivyo kwa wasanii walio wengi kwa sasa, iliweza kumrudisha nyuma kimaendeleo kwa miaka hiyo miwili . Baada ya muda kupita alijitangaza kufanikiwa kuacha matumizi hayo ya madawa makali yakulevya, na kusema kuwa kutumia muda mwingi katika ibada. “Sala, kusoma vitabu na kujiweka mbali na makundi mabaya ndio kumenisaidia kuacha kutumia madawa”, alisema qchief alipokuwa anaelezea kile kilichokuwa kinamsaidia hadi kufanikiwa kuachana na mswala hayo ya madawa yakulevya.Hadi hivi sasa qchilla yupo fiti na kurudi katika muziki wa bongo fleva.

Aisha madinda:
Aisha Mbegu ‘Madinda’ ni msanii mwingine wa muziki wa dansi aliyewahi kukiri kusumbuliwa na matatizo ya matumizi ya dawa ya kulevya,yeye akiwa amesumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu kidogo,aliweza kukiri kuwa matumizi ya madawa yalimpelekea kupoteza ramani ya maisha kabisa,nakujikuta kurudi nyuma kimuziki.

Aisha madinda baada ya kuona kuwa,hakuna kinachoenda sawa katika mipango yake kimaisha, aliamua kwenda kutafuta utatuzi huo,nakujisalimisha katika hospitali ya taifa ya muhimbili, ndipo alipoweza kupata matibabu yake ambayo hadi sasa kufanikiwa kuacha kabisa matumizo hayo.Kutokana na juhudi zake za kupambana na madawa hayo aliweza kupata kazi ya uhamasishaji ,katika shirika la Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ukimwi(PHRP),iliyopo huko Kinondoni,kazi kubwa aliyokuwa nayo ni kutoa somo juu ya matumizi ya dawa za kulevya na athari zake na jinsi yakuziacha kwa waathirika waishio katika kituo hicho.
Ray c.
I broke up with my ex,nikasema kwanza nimtoe huyu aliyeniletea balaa hili.Haata mama yangu aliona mabadiliko.I loved him so much woth all my heart,but then I had to let him,ilibidi aende cause yeye ndiye aliyeniletea balaa lote”alikiri ray C akielezea kile kilichosababisha yeye kuingia katika janga hili la madawa ya kulevya .Ray c ni mwanamuziki mkubwa sana katika ramani ya Bongo fleva, aliyeweza kushika nyoyo za mashabiki wengi wa kila rika,mbali na ujuzi wake wa kukata(kucheza) ,pia ni sauti yake ile nzuri ya kumtoa nyoka pangoni ,kitu kinachopelekea kuwa na mashabiki wengi wa kila pembe za Africa ya mashariki.

Baada ya kujihusisha na maswala ya madawa,Ray c anakiri kuwa,alianza kuona mambo yake hayaendi sawa ,na kila afanyalo hafanikiwi,wakati yeye mwenyewe ni mwanamke wa kazi,ikabidi atafakari na kuanza harakati ya jinsi ya kutatua tatizo lake kwa kuwa alishajitambua kuwa madawa ya kulevya ndio yanayomrudisha nyuma kimaendeleo.
Ilikuwa si kazi rahisi kwake Ray C kupigana na gonjwa hilo,jambo lilomfanya kuhaha kila kona kutafuta matibabu,yaliyompeleka hadi Nairobi na baadaye kurudi hapa nchini Tanzania na kufanikiwa kupata matibabu katika hospitali yataifa yaliyompa matunda makubwa na hatua kubwa katika kupigana na ugonjwa huo.Hadi hivi sasa Ray c ameacha kabisa matumizi hayo na kufanikiwa kuanzisha Foundation yake mwenyewe ,inayosaidia waathirika wa madawa ya kulevya.

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI..


Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved