TAJIRI NAMBA MOJA DUNIANI ATUA ARUSHA... BAJETI YAKE NI MARA NNE YA TANZANIA, AONGOZANA NA WATU 50 KIMYA KIMYA BILA MBWEMBWE

Monday, March 3, 20140 comments



TAJIRI namba moja duniani, Bw. Mukesh Ambani (53) (pichani) raia wa India amewasili nchini jana alfajiri kimyakimya kwa safari ya
kitalii.

Tajiri huyo aliwasili juzi saa 10.15 alifajiri Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na ndege nne binafsi akifuatana na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 50.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na mmoja wa waratibu wa safari hiyo hapa nchini, Bw. Godfrey Famandes zimeeleza kuwa lengo la safari yake ni kutembelea hifadhi za taifa, hususan Hifadhi ya Serengeti.


Bw. Ambani kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya kimataifa ndiye tajiri namba moja akimiliki dola za Marekani bilioni 63.2 (zaidi ya sh. trilioni 90), akifuatiwa na Carlos Slim Helu kutoka Mexico mwenye dola za Kimarekani bilioni 62.2993 na Mmarekani William
Bill Gates akifuatia kwa karibu akimiliki dola za Marekani bilioni 62.29.

Katika kundi hilo dogo la matajiri watano duniani nafasi ya nne inashikiliwa na
Warren Buffett kutoka Mexico ambaye anamiliki dola 55.9 na kufuatiwa na Lakshmi Mittal wa India mwenye kitita cha dola bilioni 50.9.
 
Akizungumza na njia ya simu jana, Bw. Famendes ambaye ni Mkuu wa Oparesheni wa Kampuni ya Gapco Tanzania ambaye pia ndiye msemaji wa kampuni hiyo na mwenyeji wa
tajiri huyo, alikiri kuwasili kwa tajiri huyo na kusita kuzungumzia safari hiyo zaidi.

 Safari yenyewe ni ya binafsi zaidi, hivyo sina cha kukueleza zaidi ya kukuthibitishia kuwa ni kweli amewasiliĆ¢€¦sina uhakika na idadi ya wafanyabiashara aliofuatana nao, alisema Bw. Famendes kwa njia ya simu.

Habari zaidi kuhusiana na safari hiyo zimeeleza kuwa tajiri huyo pamoja na wenzake wamewasili Hifadhi ya Serengeti, ambayo ina hadhi ya urithi wa dunia, na tayari jana walifanya mzunguko wa kwanza wa kutembelea hifadhi hiyo na kujionea maajabu ya dunia ya hifadhi hiyo.
 
 Kuja kwa mfanyabiashara huyo na wenzake na fahari kubwa kwa Tanzania, kwani ni kielelezo kuwa tayari dunia imeanza kujua vivutio tulivyo navyo, nchini na umuhimu wake duniani, alisema mmoja wa wakurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) huku akisizitiza kuwa hana habari lakini akiahidi kufuatilia ujio huo.

Bw. Ambani alizaliwa Aprili 19 mwaka 1957, huko Aden (Colony of Eden) sasa Yemen akiwa na uraia wa India. Kwa sasa anaishi Antilia,
Mumbai Maharashtra na mke wake Nita Ambani, wakiwa na watoto watatu, Akash, Anant na Isha

Alisoma Chuo Kikuu cha Mumbai na baadaye Stanford, Uingereza. Kwa sasa ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reliance Industries chini ya Ambani Group of Campanies. 
 
 
CHANZO: MAJIRA

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved