Ommy akiwa na Sofia Skvortsova
“Kwanza yule msichana wakati mimi natoka naelekea location, tupo kwenye taa hivi ambapo tunavuka taa ambazo ukizivuka unaelekea eneo la location nikawa namuona msichana yaani mzuri halafu nikawa nasema kimoyomoyo kwasababu nilikuwa sijamuona nikakutana naye location moja kwa moja, hatukukutana siku ya kwanza tukapanda, hapana, alikuja moja kwa moja siku ya kushoot,” Ommy ameiambia Bongo5.
Amesema baada ya kumuona Sofia alimwambia mshkaji wake kuwa anatamani msichana kama huyo awe kwenye video yake. Ameongeza kuwa siku ya kufanya video alipofika location akamkuta Sofia eneo hilo na kumchanganya zaidi Ommy.
“Baadaye Moe Musa ndio ananiita ananitambulisha ‘huyu ndio video model, sijui unamuonaje,” ameelezea Ommy. “Mimi nikamwambia, ‘mimi nimempenda sana’ mimi nilimuambia nataka msichana mzuri kulingana na uzuri wa nyimbo na maadhui ya nyimbo yalihitaji msichana mzuri.”
Ommy amesema kama mambo yakienda sawa anafikiria kumleta Sofia Tanzania siku ya uzinduzi wa video hiyo. Tangu amtambulishe kwenye Instagram, Sofia amepata followers wengi kutoka Tanzania. “Alipata followers wengi kutoka huku kwahiyo akashangaa sana halafu akaappreciate.”
Msikilize Ommy hapa:
Post a Comment