Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo, Priscus Mallya, baada ya kufariki katika ajali ya lori na Bajaj.
MWANAFUNZI wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Makongo, Priscus
Mallya, amefariki dunia katika ajali iliyolihusisha lori na Bajaj katika
barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la Bamaga, Dar.
Kwa mujibu wa watu waliokuwa eneo la tukio wakati ajali hiyo
ikitokea, wamesema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ndani ya Bajaj pamoja na
wenzake wawili wakielekea shuleni Makongo ambapo walikutana uso kwa uso
na lori kisha kumrusha na kutokea upande wa pili marehemu.
Post a Comment