Bwana
mmoja huko mbezi beach amemrudisha mkewe nyumbani ajiwa mahututi badala
ya kumpeleka hospital kubwa ya Mwananyamala kama rufaa ilivyoandikwa na
madaktari wa Masana Hospital iliyoko Mbezi jijini Dar (Afande Jaina
Msangi, kushoto, dada wa mgonjwa Ramla kulia kwa mgonjwa, mimi mbele ya
mgonjwa wakati tukimbeba kwa ajili ya kumpeleka Mwananyamala. Kushoto
kabisa ni mume wa mgonjwa akiwa pembeni kabisa
Huyo
ndo Mume wa mama Linda Mgonjwa, hapo akituambia hataki presha kama
tunataka kumpeleka hospital tumchukue....baada ya vuta nikuvute ya
kumtoa mgonjwa nyumbani apelekwe mwananyamala hatimae tulifanikiwa, na
huyu mzee hajaenda kumuona tangu ampeleke...
Wakati tunahangaika kumbeba mke wake tumweke kwenye gari, yeye hatoi kabisa ushirikiano ndo kwanza yupo buze na mambo yake.
Tukamkomalia ndo akasaidia.!!!
Nikamuulia NIA yake ya kumrudisha Mgonjwa asiyejitambua tena ni Mke wake, alikuwa na Lengo gani?
Hapa ndo nyumbani kwa huyu mzee na mke we Linda Msoka. Huyu mama mpaka sasa ni mfanyakazi wa Hazina.
Huyo
gumegume alikuwa anafanyakazi Kiwanda sijui gani inavyoonekana mama ndo
yuko vizuri kiuchumi, na mpaka sasa ni mfanyakazi wa Hazina lakini
analala njaa yeye na huyu binti anaemsaidia Haya majumba mazuri jamani
yana tabu? Heri sie tunakaa tandale kwa Amani
Linda
Amekaa Mwananyamala siku sita leo siku ya saba tumemwamishia Muhimbili.
Huyu mzee mume wake kaja siku mbili tu kati ya hizo siku sita, jana
tulimwambia kwamba mgonjwa atahamishiwa Muhimbili akasema hataki
usumbufu kama anahamishiwa huko yeye haimuhusu....
Post a Comment