Picha
iliyotolewa na vyombo vya habari vya China vikionyesha kitu kipya
kilichogunduliwa na satellite za nchi hiyo kikielea katika Bahari ya
Hindi ambacho kinahisiwa huenda kikawa na uhusiano na ndege ya Malaysia
iliyopotea.
Picha
za Satellite kutoka kituo cha utafiti cha Marekani kikionyesha eneo
ambako msako mkali unaendelea kuitafuta ndege iliyopotea huko katika
bahari ya Hindi.
Hussein
aliwaambia waandishi wa habari jijini Kuala Lumpur: 'Balozi wa China
amepokea picha ya kitu kinachoelea kusini mwa bahari ya Hindi na amesema
watatuma meli kuchunguza.
Ofisa
wa anga, Peter Moore, ambaye pia ni rubani, amesema mchanganyiko wa
hali ya hewa nchi kavu na ile ya bahari unaathiri ndege za uokoaji.
• Waziri wa Mawasiliano Malaysia atangaza picha mpya ya Satellite• Asema China imetuma meli kuchunguza
• Ni wiki mbili sasa tokea ndege hiyo ipotee
Kipande kikubwa cha chuma kimeonekana kikielea katika bahatri ya Hindi. Picha za Satellite za China zimeona kipande chenye urefu wa futi 72 kiasi cha maili 75 mashariki mwa Australia.
Picha hizo zimechukuliwa siku mbili tu baada ya mamlaka za Australia kuona kitu kinachoelea katika pwani ya bahari ya Hindi.
Post a Comment