MSANII
chipukizi wa maigizo nchini, Calvin Ponella anayeshiriki Tamthiliya ya
Millosis inayoendelea katika Runinga ya TBC 1, ametelekezewa mtoto wa
kike aitwaye Naomi na mzazi mwenzake aitwaye Diana.
Hivi ninavyozungumza na wewe suala lao limefikishwa Ustawi wa Jamii hapa Morogoro,” kilipasha chanzo chetu.
Paparazi wetu alifunga safari hadi zilipo Ofisi za Ustawi wa Jamii, mjini hapa na kufanikiwa kumkuta msanii huyo akiwa na mtoto wake, baada ya kufikisha shauri hilo katika chombo hicho cha kutetea masilahi ya jamii.
Akizungumza na Ijumaa, mmoja wa maofisa wa Ustawi wa Jamii aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mkapa alisema ni kweli shauri hilo limefika mikononi mwake lakini wamelimaliza kwa njia ya mazungumzo bila kufafanua zaidi.
Kwa upande wake Calvin alisema: “Hii ishu inanitesa sana, ni kweli kuna tofauti kidogo na mwenzangu lakini hatua aliyoichukua ni kubwa sana. Najipanga kwenda kumuangukia ili tuyamalize.”
Post a Comment