NORA AMUANIKA MPENZI WAKE MPYA MTANDAONI...BAADA YA SIKU CHECHE SANA KUMWAGWA NA MPENZI WAKE AMBAYE NI MSANII MWENZAKE

Wednesday, October 16, 20130 comments

Nuru Nassor ‘Nora’ akiwa na mwanaume mpya.
SIKU chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Nuru Nassor ‘Nora’ kumwagana na mpenzi wake Geofrey Kusila, sasa amezua gumzo baada ya kuibuka na mwanaume mwingine mtandaoni.
 
Risasi Mchanganyiko limenasa picha ya Nora akiwa amepozi na mwanaume huyo ambaye jina lake halijapatikana huku pembeni kukiwa na mbwa, katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram ikisindikizwa na maneno: “...na mlivyosawigika kama huyu mbwa, mjipange nina hasira na nyinyi hadi Mungu anajua.”
Paparazi wetu alivyomtafuta kwa njia ya simu, Nora alisema: “Mimi ni mwanamke hivyo kuwa na mpenzi ni lazima na huyo uliyemuona ni mwanaume, hivyo haina haja ya kujibu na kuhusu anaitwa nani hiyo ni siri yangu, siwezi kuweka wazi jina lake kwa sasa.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved