MNENGUAJI wa kiume wa Mashujaa Band, Juma
Nyamwela (Nyamwela Jr) amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumlawiti
mtoto wa kiume wa umri wa miaka sita.
Kwa sasa mnenguaji huyo (pichani wa tatu kutoka kulia waliochuchumaa) yupo kituo cha polisi cha Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya tatu tangu akamatwe kwa tuhuma hizo.
Habari za uhakika kutoka kituoni hapo zinasema katika maelezo ya awali, mnenguaji huyo amekiri kosa.

Super Nyamwela
Chanzo kimeeleza kuwa huenda mnenguaji huyo akafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.
Nyamwela ambaye ni mdogo wake na Super Nyamwela wa Extra Bongo, aliwahi kuitumikia TOT Plus kabla ya kujiunga na Mashujaa Band. Mwaka 2007 aliibuka bingwa wa mashindano ya dansa bora wa kiume yaliyoandaliwa na Usher Family na kujinyakulia zawadi ya gari.
-SALUTE 5.