Msanii mdogo aliyewahi
kutamba katika tasnia ya muziki wa bongo fleva Dogo Janja amefukuzwa
rasmi Mtanashati Entertinment, Taarifa zilizofikia dawati letu la habari
zinasema Dogo Janja amefukuzwa na Ostazi Juma Na Musoma baada ya
kushindwana kitabia, Hapo awali Dogo Janja aliwahi kuwa mwanakundi la
Tip Top Connection lililo chini ya uongozi wa Madee hata hivyo
alifukuzwa na kurudi kwao Arusha ambapo Ustazi Juma Na Musoma alimfuata
na na kumuweka kundini huku akimuhudumia katika kila jambo ambalo
alitakiwa kupata kama
mtoto na mwanamuziki pia. Lakini Leo imefika
tamati ya Ostazi Juma na kuamua kumuacha Dogo Janja aende zake.
Vile vile kutoka katika
kundi hilo la Mtanashati Kuna nyimbo mpya ya msanii PNC inayokuja hivi
karibuni, ni Bonge moja la track linakwenda kwa jina la HABARI YA MJINI,
nyimbo hii itayoachiwa hvi karibuni itakuja pamoja na video kali.
Jiandae kwa nyimbo kali kutoka kwa PNC
Post a Comment