DINI MPYA YA AJABU ILIYOANZISHWA HUKO MBEYA INAWAFAA WENGI.SOMA HAPA UJIONEE MAAJABU...

Friday, October 25, 20130 comments

Dini inayoamini katika MUNGU lakini ikiruhusu yale ambayo dini zingine zinapinga imeanzishwa eneo la mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya,


Dini hiyo haiamini katika kutoa sadaka bali inasema tunamtolea nani sadaka wakati Vitu vyote tulivyonavyo ni mali ya MUNGU,kwa nini tunampa MUNGU mali zake Mwnyewe.!

Dini hiyo inaruhusu ulevi,uchawi na uzinzi kwa sababu vimeumbwa na MUNGU,Vile vile inaamini hakuna dhambi duniani,Dini hiyo inaitwa DIMAYO, sasa imeanza kuenezwa Mbeya

=========================
Ufafanuzi
=========================
By GAMBISHI DWESE
Yawezekana kweli Bwana Domy umekutana nami. Mimi Ndiyo PAPA-DIMAYO 1: GAMBISHI DWESE,( nabii wa kwanza wa DIMAYO) hata hivyo pengine umeninukuu kimakosa.Kwanza kabisa Dimayo haiamini katika uwepo wa mungu muumbaji aliye hai wala aliyekufa anayedaiwa kuhusika na kila kinachoendelea ulimwenguni.

Na nimeshatoa kitabu kinachoitwa HAKIKA HAKUNA MUNGU MUUMBAJI ALIYE HAI WALA ALIYEKUFA anayehusika na kila kinachoendelea. kijitabu hiki kinaeleza kinagaubaga kwanini Dimayo haiamini katika uwepo wa mungu muuumbaji. nikipata nafasi nitakiingiza kwenye mtandao ili watu wengi wakisome.

Ni kweli hakuna kitu Dhambi bali kuna makosa. na kosa linaweza kuwa kosa kulingana na mazingira na wakati katika jamii tofauti. Na ni kweli kwamba dini yetu ni ya starehe wala si ya mateso, maana tunaamini hakuna maisha zaidi ya haya tuliyonayo. Dimayo haijampa mtu ruksa ya kuvunja kanuni halisi asili wala sheria halali ya serikali yake halali na wala haina upotoshaji hata kidogo. 

Kinachoitwa sadaka kwetu huwapa watu wenye matatizo. Ni kweli kuna michango mingine lakini ni ya hiari na ni kwa ajili ya ushirika. Ni kweli kwenye JUMADI (jumba la makutano la Dimayo kutakuwa na kaunta ya vinywaji). unajua kunywa na ulevi ni vitu viwili tofauti; ulevi ni tabia ya mtu ya kutumia vileo kupindukia, lakini kwetu tunasema kunywa uwezavyo ilimradi huumii wala kuumiza vyote kisaikolojia na kimwili, kwa mantiki hiyo ulevi kwetu noma ila unywaji ni safi.

Uchawi ni sayansi, ila utumike kwa faida siyo kwa kuleta madhara. kuwaambia watu eti acheni ngono eti mungu hapendi wataacha?. wambie wafanyeje ngono kulingana na wakati na mazingira. Dimayo inamfundisha mtu kutenda inavyofaa yanayofaa kutendwa kwa kufuata kha na kahaka.

Anyway nashukuru kwa kuianzisha mada hii, nafikiri nitachukua nafasi kuielezea zaidi kila inavyowezekana.
Nina uhakika kwa mtu yeyote mwenye uwezo mkubwa wa kutumia akili zake hawezi kupingana hata kidogo na DIMAYO.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved