RIDHIWANI KIKWETE APIGA KAMPENI KATIKA KATA YA FUKAYOSE JIMBONI CHALINZE‏

Sunday, March 23, 20140 comments


2
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayose Jimbo la Chalinze jana.
3
Mwenyekiti wa kata ya Fukayose, Orinjulie Machanga akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mkenge wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete.
4
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa wameshikilia picha za mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Bw. Ridhiwani Kikwete katika mkutano wa kampeni kijiji cha Mkenge.
5
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mkenge mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni kijijini hapo.
6
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze, Bw. Ridhiwani Kikwete akihani msiba katika moja ya kijiji kwenye kata ya Fukayose.
1
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika kata ya Fukayose Jimbo la Chalinze wakati alipoendelea na mikutano ya kampeni kuwania kiti cha ubunge jimbo la kata hilo. Ridhiwani Kikwete amewaomba wananchi wa kata ya Fukayose kumuamini na kumpa kura za ndiyo siku ya Jumapili Aprili 6 mwaka huu na yeye atawalipa maendeleo na watapata nafasi ya kupanga mipango ya maendelea kwa ajili ya mafanikio ya Jimbo la Chalinze.
7
Msanii Dokii akitumbuiza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Fukayose jana.
8
Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni meneja wa kampeni wa mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM, Bw. Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi katika kata ya Fukayose.
9
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano.
116
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze, Bw. Ridhiwani Kikwete, akizungumza na kuwapa pole wafiwa wakati alipohani msiba katika moja ya kijiji kwenye kata ya Fukayose.
12
Msanii Hafsa Kazinja akitumbuiza katika moja ya mikutano hiyo ya kampeni iliyofanyika kwenye kata ya Fukayose.
13Askari Polisi akiimarisha ulinzi katika mkutano huo huku baadhi ya vijana wa Kimasai wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali katika mkutano huo.
14
Mmoja wa wazee ambaye jina lake halikufahamika mara moja katika kijiji cha Mtakuja akiwa ameshikilia kipeperushi chenye picha na maelezo ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia CCM Bw. Ridhiwani Kikwete.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved