OMMY DIMPOZ AKUTANA NA MREMBO KWENYE VIDEO YAKE MPYA NA AMEPANGA KUMTAMBULISHA SIKU YA UZINDUZI...MSIKIE MWENYEWE HAPA

Monday, March 17, 20140 comments

Ommy Dimpoz amesema kabla hata ya kufahamu kuwa Sofia Skvortsova ndiye model atakayemtumia kwenye video yake, alikuwa amemuona na akatamani msichana kama yeye aonekane kwenye video hiyo.
e61e0e96a8e611e3bd540e4cd1fa8f5b_8
Ommy akiwa na Sofia Skvortsova
“Kwanza yule msichana wakati mimi natoka naelekea location, tupo kwenye taa hivi ambapo tunavuka taa ambazo ukizivuka unaelekea eneo la location nikawa namuona msichana yaani mzuri halafu nikawa nasema kimoyomoyo kwasababu nilikuwa sijamuona nikakutana naye location moja kwa moja, hatukukutana siku ya kwanza tukapanda, hapana, alikuja moja kwa moja siku ya kushoot,” Ommy ameiambia Bongo5.
7cf829e4a60511e3a5b712a3de486cc5_8
Amesema baada ya kumuona Sofia alimwambia mshkaji wake kuwa anatamani msichana kama huyo awe kwenye video yake. Ameongeza kuwa siku ya kufanya video alipofika location akamkuta Sofia eneo hilo na kumchanganya zaidi Ommy.
“Baadaye Moe Musa ndio ananiita ananitambulisha ‘huyu ndio video model, sijui unamuonaje,” ameelezea Ommy. “Mimi nikamwambia, ‘mimi nimempenda sana’ mimi nilimuambia nataka msichana mzuri kulingana na uzuri wa nyimbo na maadhui ya nyimbo yalihitaji msichana mzuri.”
01
Ommy amesema kama mambo yakienda sawa anafikiria kumleta Sofia Tanzania siku ya uzinduzi wa video hiyo. Tangu amtambulishe kwenye Instagram, Sofia amepata followers wengi kutoka Tanzania. “Alipata followers wengi kutoka huku kwahiyo akashangaa sana halafu akaappreciate.”
Msikilize Ommy hapa:
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved