HUYU NDIO MSANII WA MAIGIZO ALIYETELEKEZEWA MTOTO...

Friday, November 8, 20130 comments

MSANII chipukizi wa maigizo nchini, Calvin Ponella anayeshiriki Tamthiliya ya Millosis inayoendelea katika Runinga ya TBC 1, ametelekezewa mtoto wa kike aitwaye Naomi na  mzazi mwenzake aitwaye Diana.
 
 Calvin Ponella.
Habari kutoka kwa mpashaji wetu, zinasema Diana aliamua kumbwagia Calvin mtoto wake kutokana na kupishana Kiswahili. “Jamaa anahaha na mtoto mitaani. Mtoto mwenyewe ni mdogo, hebu fikiria ana mwaka mmoja na nusu tu, halafu ni wa kike, atawezaje kumlea mwenyewe?

Hivi ninavyozungumza na wewe suala lao limefikishwa Ustawi wa  Jamii hapa Morogoro,” kilipasha chanzo chetu.
Paparazi wetu alifunga safari hadi zilipo Ofisi za Ustawi wa Jamii, mjini hapa na kufanikiwa kumkuta msanii huyo akiwa na mtoto wake, baada ya kufikisha shauri hilo katika chombo hicho cha kutetea masilahi ya jamii.
Akizungumza na Ijumaa, mmoja wa maofisa wa Ustawi wa Jamii aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mkapa alisema ni kweli shauri hilo limefika mikononi mwake lakini wamelimaliza kwa njia ya mazungumzo bila kufafanua zaidi.
Kwa upande wake Calvin alisema: “Hii ishu  inanitesa sana, ni kweli kuna tofauti kidogo na mwenzangu lakini hatua aliyoichukua ni kubwa sana. Najipanga kwenda kumuangukia ili tuyamalize.”


Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. NDANI YA JAMII - All Rights Reserved